Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Katibu Mkuu atembelea NSSF


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu Bi. Mary Maganga amekutana na Menejimenti ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea Ofisi za NSSF Dar es Salaam.

Aidha, amepongeza kazi kubwa inayofanywa na NSSF katika kutekeleza majukumu yake ambayo ni kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao.