Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Katambi: Vijana 101,579 wamepata mafunzo kwa njia ya uanagenzi


NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Vijana Ajira na wenye Ulemavu, Mhe Patrobas Katambi amesema serikali kupitia programu ya Taifa ya ukuzaji ujuzi nchini tangu kuanza utekelezaji wake mwaka 2016/17 imewezesha jumla ya vijana 101,579 kupata mafunzo kwa njia ya uanagenzi.

Mhe Katambi ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Tunza Issa Malapo aliyehoji Serikali inawasaidiaje wanaomaliza VETA na Vyuo vingine vya Ufundi kupata mitaji.

Amesema mafunzo hayo yamekua yakifanyika kupitia vyuo mbalimbali vya ufundi vya serikali na binafsi ambavyo vimewezesha vijana kupata mafunzo ya ufugaji wa viumbe maji kupitia taasisi za serikali na binafsi na kuwawezesha vijana kupata mafunzo ya unenepeshaji mifugo kupitia taasisi za serikali na binafsi.

“ Kati ya vijana 101,579 walionufaika na mafunzo ya uanagenzi vikundi vya vijana 219 vyenye jumla ya vijana 1,621 vimewezeshwa vifaa mtaji kwa ajili ya kuendeleza ujuzi walioupata"

Katambi abainisha kuwa Vikundi vya vijana 118 vyenye vijana 100 vimewezeshwa cherehani 372. Vikundi vya vijana 56 vyenye vijana 369 vimewezeshwa vifaa vya uchomeleaji seti 65, na vikundi 45 vyenye vijana 58 vimewezeshwa vifaa vya kutengeneza bidhaa za aluminium seti 58.