Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kampeni kupinga ukatili dhidi ya Wenye Ualbino yazinduliwa


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Deogratius Ndejembi amezindua kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya Watu wenye Ualbino inayolenga kulinda haki zao sambamba na kukuza ustawi wa kundi hilo.

Aidha, Kampeni hiyo ya kupinga ukatili dhidi ya watu Wenye Ualbino ambayo ilikuwa na kauli mbiu “Mimi nipo na Mama Samia Suluhu Hassan ninapinga ukatili dhidi ya watu Wenye Ualbino”

Mhe. Ndejembi amezindua kampeni hiyo Julai 12, 2024 ambapo amewataka Wakuu hao wa Mikoa kuhakikisha wanafanya kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya watu wenye Ualbino katika Halmashauri zote na kuhakikisha kamati za watu wenye ulemavu zinaimarishwa katika maeneo yao kwani ni takwa la kisheria kupitia sheria namba 19 ya mwaka 2010 ya watu Wenye Ulemavu.

Kwa upande mwengine, Mhe. Ndejembi ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa huo kuwa Mabalozi wa ulinzi wa Mtu Mwenye Ualbino kwa kutoa elimu, kupinga ukatili na kutoa taarifa kwa viongzo pale wanaposikia ama kuona viashiria vya ukatili dhidi ya watu hao.

Awali akizungumza Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassi amesema ataendelea kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama kuhakikisha vitendo vya kikatili dhidi ya Wenye Ualbino vinakomeshwa Mkoani humo.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania Alfred Kapole ameishukuru serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusimamia kundi la Watu Wenye Ualbino ikiwa ni pamoja na kuwasaidia vifaa kinga.