Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kamati ya Bunge Yaridhishwa Kazi ya Ujenzi Kiwanda cha Sukari Mkulazi


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatma Taufiq amesema kwa niaba ya kamati hiyo ameridhishwa na ujenzi wa kiwanda cha Sukari Mkulazi ambao umefikia 89%.

Amefafanua kuwa kukamilika kwa kiwanda hicho kutapunguza changamoto ya ukosefu wa sukari kwa matumizi ya binadamu na viwandani ambapo kitazalisha tani 50,000 kwa siku.

"Pamoja na kutatua changamoto ya ajira, zaidi ya vijana 2000 nchini wanatarajia kunufaika na ujenzi wa kiwanda hicho kwa kupatiwa ajira kulingana na ujuzi wao"

Ameyabainisha hayo Februari 14,2023 wakati kamati hiyo ilipotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanda.

Mwenyekititi huyo ampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt..Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kutoa fedha kwa ajili ya ujezi wa kiwanda.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Prof. Joyce ndalichako amesema lengo la serikali ni kuhakikisha inaimalisha uzalishaji wa viwanda, kupunguza upungufu wa sukari nchini na kutoa fursa kwa watanzania kupata ajira hususani vijana.

Amewataka wakandarasi kukamilisha ujezi wa kiwanda hicho kwa wakati ili kianze kufanya kazi kwa wakati ifikapo Julai mwaka huu.

Naye Mtendaji Mkuu wa Kiwanda hicho, Selestine Some, amesema mradi huo hadi kukamilika utagharimu shilingi bilioni 344.47 na kufikia februari 28 mwaka huu jumla ya fedha zilizotolewa kama mtaji ni shiling bilioni 263.60 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 19.38 ni thamani ya ardhi na shilingi bilioni 127.00 fedha taslimu kwa ajili ya kazi ya kilimo cha miwa.

Hadi kufikia Februari 2023 mradi huo umetoa ajira kwa wafanyakazi 1,025 kati ya hao,wafanyakazi 340 wanafanya kazi za ujenzi wa kiwanda, 450 wanafanya kazi za mashambani na kitakapokamilika kitaajiri wafanyakazi zaidi ya 2315.

Kamati hiyo pia, imetembelea kiwanda cha nyama cha Ngulu hills na kukagua maendeleo ya kiwanda hicho na kukiri kuridhishwa na maendeleo ya kiwanda hicho yaliyofikia asilimia 98.