Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

Announcement

Vigezo vya Kupata Wajasiriamali Maonesho ya 23 Nguvukazi / Jua Kali


  • VIGEZO
1. Mshiriki mwenye kuzalisha bidhaa zenye ubora na kukidhi viwango vinavyokubalika kibiashara na watakaotoa sura halisi ya bidhaa zinazotengenezwa Tanzania hususan katika Mkoa husika;
2. Mshiriki awe na vipeperushi na kadi ya utambulisho wa bidhaa (business cards) kama nyenzo muhimu ya kutangaza bidhaa na kutafuta masoko;
3.Mshiriki awe na bidhaa za ubunifu wa hali ya juu, kipaumbele ikiwa ni bidhaa zinazotokana na ngozi na mazao ya ngozi, nguo pamoja na bidhaa za kilimo zilizosindikwa, mifugo, Bahari, viungo (spices) na urembo;
4.Mshiriki awe na cheti cha uasili wa bidhaa (Certificate of origin)kinachotolewa na TCCIA na ZCCIA kwa upande wa Zanzibar;
5.Mshiriki awe na vifungashio vizuri vya bidhaa yake vinavyokubalika kimazingira;
6.Wale ambao bidhaa/huduma zao zinaonesha utamaduni wa kitanzania au Mkoa husika na hivyo kuwa kivutio cha wawekezaji, wanunuzi au watumiaji wa bidhaa/huduma hizo;
7.Wale wenye huduma/bidhaa zenye ubora wa kipekee na kuonesha ubunifu kama vile bidhaa/huduma zinazotengenezwa kwa mikono, mbao, mashine, vipuri, bidhaa za usindikaji, bidhaa za sanaa, teknolojia (E-marketing) na nyinginezo zinazoweza kutumika viwandani, majumbani na maofini;
8.Mshiriki anayejihusisha na bidhaa za vyakula, dawa na vipodozi awe na uthibitisho wa kibali cha kusafirisha bidhaa husika nje ya nchi (export permit) kutoka TFDA au ZFDA kwa upande wa Zanzibar;
9.Mshiriki awe tayari kujaza dodoso la taarifa za maendeleo ya biashara yake wakati wa Maonesho kama itakavyotakiwa na kurejesha dodoso kwa waratibu wa maonesho; na
10. Mshiriki awe na uwezo wa kujihudumia muda wote wa maonesho na kujigharamia usafiri kwenda na kurudi nchini Burundi.
FOMU YA USAJILI KWA WAJASIRIAMALI WATAKAOSHIRIKI KWENYE MAONESHO YA 23 YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (NGUVU KAZI/JUA KALI) YATAKAYOFANYIKA BUJUMBURA, BURUNDI KUANZIA TAREHE 05 - 15 DESEMBA,2023

Bonyeza Kupakuwa Fomu: https://www.kazi.go.tz/uploads/documents/en-1699342791-Fomu%20ya%20wajasiriamali%202023.pdf