Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ridhiwani Kikwete akutana na TUGHE, Taasisi ya Doris Mollel Foundation


Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwan Kikwete amekutana na kuzungumza na viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) na Taasisi ya Doris Mollel Foundation tarehe 15 Agosti, 2024 Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.

Katika kikao hicho, pamoja na mambo mengine walipata nafasi ya kujadili masuala mbalimbali ya Wafanyakazi ikiwemo suala la nyongeza ya siku za likizo ya Uzazi kwa wafanyakazi wanaojifungua watoto njiti.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara hiyo, Zuhura Yunus, Kaimu Naibu Mkuu wa TUCTA, Said Wamba na Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE, Rugemalira Rutatina.