Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ridhiwani atoa maagizo matatu WCF


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ametoa maagizo mahsusi matatu kwa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ili uweze kuilinda nguvu kazi ya Taifa

Akizungumza na wafanyakazi wa Mfuko huo leo Februari 20, 2025 jijini Dar es salaam, Ridhiwani ameuagiza mfuko huo kusajili waajiri wote nchini kwa asilimia 100 pindi unapoanza mwaka mpya wa fedha 2025/26 kwa kuwa kwa sasa usajili huo umefikia asilimia 93.

Pia, ameuelekeza Mfuko huo kuendelea na uwekezaji wenye tija hususani katika hatifungani ili fedha za wanachama zilete tija katika utoaji wa mafao.

Aidha, Mhe. Ridhiwani amesisitiza kufanya kazi kwa ufanisi kwenye utekelezaji wa majukumu yao.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt.John Mduma, amemhakikishia Mhe. Waziri kutekeleza maagizo hayo na amebainisha kuwa mfuko huo utaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ikiwemo kukusanya michango, kuwekeza, kulipa fidia na kulinda nguvu kazi ya watanzania.