Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Wananchi waendelea kujitokeza kwa wingi banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Maonesho ya nanenane Dodoma


Wakazi wa Mkoa wa Dodoma na kutoka mikoa ya jirani wamekuwa na mwitikio mkubwa wa kutembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa ajili ya kupata huduma na uelewa wa masuala mbalimbali yanayotekelezwa na ofisi hiyo.

Aidha, katika maonesho hayo Ofisi ya Waziri Mkuu inashiriki pamoja na Taasisi zake na imeendelea kuwaelimisha na kuwafahamisha wananchi na wadau juu ya masuala mbalimbali yanayotekelezwa na ofisi hiyo ikiwemo masuala ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Ajira na Ukuzaji Ujuzi, Ustawi wa Watu wenye Ulemavu, Hifadhi ya Jamii, Uratibu wa Maafa, Uratibu wa shughuli za Serikali.

Vile vile, masuala ya Ufuatiliaji na tathmini za shughuli za Serikali, Sheria za Uchaguzi, udhibiti wa ukimwi, udhibiti wa dawa za kulevya na fursa za uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa (Nanenane) yalifunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Agosti Mosi, 2024 jijini Dodoma ambapo maonesho hayo yanafanyika kitaifa huku yakiongozwa na kauli mbiu isemayo: " Chagua Viongozi bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi,"