News
Ridhiwani Kikwete afanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Nchini Uholanzi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Nchini Uholanzi leo Novemba 13, 2024 Jijini Dar es salaam.
Aidha, lengo kukutana ni kujadili namna ya kuwashirikisha vijana wa kitanzania katika fursa za kiuchumi ili waweze kutengeneza ajira.
Ujumbe kutoka Nchini uholanzi umeongozwa na Waziri wa Vijana, Elimu na Ajira Mhe. Jurrian Middelhoff.