News
Ridhiwani aipongeza ATE Maadhimisho Miako 10 ya Uongozi kwa Wanawake
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Ridhiwani Kikwete ameipongeza ATE kwa Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanza kwa mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake Tanzania (Female Future Program) pamoja na Mahafali ya Wahitimu wa Awamu ya 10 ya Mafunzo hayo.
Mhe. Kikwete ameipongeza ATE kwa kuendesha mafunzo hayo kwa kipindi hicho chote kwa ufanisi ambayo yanachochea ari ya Uongozi kwa Wanawake kutoka katika sekta mbalimbali nchini.
21 Februari, 2025.