News
Ofisi ya Waziri Mkuu yatoa elimu kwa wanafunzi chuo cha Maendeleo ya Jamii
Utoajia wa Elimu katika Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa unaendelea katika Maonesho hayo, ikiwa ni pamoja utoaji Elimu katika madarasa maalum Kwa ajili ya makundi mbalimbali ya kijamii, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imetoa Elimu kwa wanafunzi wanafunzi wa chuo cha Maendeleo ya Jamii (CDTI - Uyole) kilichopo Mkoani Mbeya.
Elimu iliyotolewa ni kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya vijana, Sera ya Taifa ya Maendeleo ya vijana, Umuhimu wa kuweka hakiba, Maswala ya Ulemavu, Programu ya Ukuzaji Ujuzi, Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA) pamoja na Mafunzo ya tarajali (Internship)
Aidha, Wanafunzi wa chuo hicho wameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kuweza kuwaongezea maarifa kutokana na Elimu waliyoipata ambayo itawasaidia wao kama Maafisa Maendeleo tarajali kwan wametambua namna bora ya kuleta mapinduzi ya Maendeleo kwa Vijana katika jamii.
Aidha vijana hao wamehamasishwa kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali kwa lengo la ustawi wao wa Kiuchumi.
Kauli Mbiu ya Maonesho hayo ni "Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi"