News
Mhe. Ridhiwani Kikwete azindua Bodi Mpya ya Wadhamini WCF
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amezindua Bodi mpya ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF, leo Machi 17, 2025 Jijini Dar es salaam.
Aidha, ameitaka bodi hiyo kusimamia maslahi ya Wanachama, uhai na uendelevu wa Mfuko huo pamoja na uwekezaji wenye tija.
“WCF imekuwa na mafanikio makubwa katika maeneo yote ikiwemo kuongezeka kwa thamani ya Mfuko, kuongezeka kwa ulipaji wa mafao kwa wanufaika wa Mfuko na kutumia mifumo ya TEHAMA kwa kiasi kikubwa kwenye shughuli za Mfuko hivyo kuongeza ufanisi katika utoaji huduma” amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo Renatha Rugarabamu ameahidi kuwa itatekeleza majukumu yake ipasavyo ili mfuko huo uendelee kuwa na uhimilivu wa kuendelea kuwalipa wanachama fidia
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa WCF Dkt. John Mduma, ameihakikishia bodi mpya ushirikiano wa kutosha ili kuwawezesha kutimiza wajibu wao kwa ufanisi, pia ameishukuru bodi iliyomaliza muda wake kwa kuuwezesha mfuko huo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.