News
Mhe. Ridhiwani akutana na Mtendaji Mkuu ATE
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Suzanne Ndomba-Doran aliyeongozana na Meneja wa Kanda ya Kati wa ATE, Bw. Leonard Mapha alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma, leo Agosti 16, 2024.
Mazungumzo hayo yalilenga kujitambulisha rasmi kwake na kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuhudumu katika Wizara hiyo.