Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kiwanda cha Sukari Mkulazi kutoa Ajira 11,315 - Mhe, Ridhiwani


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Kiwanda cha sukari Mkulazi kitatoa ajira 11, 315 kwa watanzania ifikapo Disemba Mwaka huu.

Aidha, amesema kukamilika kiwanda hicho kutaongeza wigo wa fursa za ajira hususan kwa vijana katika shughuli za uzalishaji kwenye kiwanda na mashamba ya miwa.


Mhe. Ridhiwani amebainisha hayo Agosti 7, 2024 Mkoani Morogoro wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi kilichozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema kuwa Ujenzi wa mradi huo umegharimu shilingi bilioni 344, ambazo zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda na kazi za kilimo, miundombinu ikiwemo ujenzi wa njia ya umeme.

"Nikupongeze Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa kipaumbele kutekeleza miradi ya kimkakati, miradi hii imekuwa chachu ya maendeleo ya taifa letu," amesema

Aidha, Mhe. Ridhiwani amemhakikishia Mhe. Rais kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kuratibu kwa karibu suala la ajira kwa vijana kwa maslahi mapana ya Taifa.

Kiwanda hicho cha sukari Mkulazi kimeanza uzalishaji rasmi Julai Mosi, 2024 na hadi sasa uzalishaji unaendelea na kwa siku kina uwezo wakuzalisha wastani wa tani za sukari 190 hadi 260