Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Katibu Mkuu Maganga akagua ujenzi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Mary Maganga amefanya ziara katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma kukagua maendeleo ya ujenzi majengo ya Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu ambao ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 83.

Akizungumza baada ya kukagua na kupata maelezo ya wataalam na wasimamizi wa jengo hilo, Katibu Mkuu Maganga amewapongeza wakandarasi kwa hatua iliyofikiwa na kuagiza majengo hayo yakabidhiwe ndani ya muda uliopangwa kwa mujibu wa mkataba ambao ni mwisho wa Mwezi Machi 2025.

Msimamizi wa Ujenzi Jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu kutoka SUMA JKT, Mhandisi Luteni Kanali Daudi Zengo ameahidi kutekeleza maelekezo hayo ili kukamilisha ujenzi na majengo yaanze kutumika kwa mujibu wa mkataba.

Naye, mwakilishi wa Mshauri elekezi wa Ujenzi huo kutoka Chuo kikuu cha Ardhi, Mkadiriaji Majenzi Anania Suden amebainisha kuwa kazi zilizobaki katika ukamilishaji wa ujenzi huo zitaendelea kufanyika kwa ufanisi na kwa wakati ili jengo hilo litumike kwa muda uliopangwa.