Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kamati ya bunge yapongeza CMA usimikaji Mfumo wa Kidijitali wa utatuzi wa Migogoro ya Kazi


✅ Yasisitiza CMA kutoa elimu kwa umma kuhusu Mfumo huo

MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Fatma Toufiq ameipongeza Tume ya Usuluhishi na Uamuzi - CMA kwa kusimika mfumo wa kidijitali wa kutatua Migogoro kwa njia ya mtandao.

Aidha, amesema Mfumo huo utasaidia kuharakisha utatuzi na usuluhishi wa migogoro kwa wakati sambamba na kuondoa kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kutatua changamoto za Watumishi.

Mhe. Toufiq amebainisha hayo leo Machi 15, 2025 alipoambatana na Wajumbe wa kamati hiyo kwa ajili ya kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Mfumo wa Usimamizi wa Uendeshaji wa Mashauri, katika Ofisi za CMA Jijini Dar es Salaam.

Vile vile, ameitaka CMA kutoa elimu ya kutosha kwa umma ili wawe na uelewa kuhusu mfumo huo unavyofanya kazi.

Katika hatua nyingine, Mhe. Toufiq amempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya shilingi Bilioni moja kusimika kwa lengo la kusimika mfumo huo, hivyo kurahisisha utatuzi wa migogoro kupitia njia ya mtandao.

Naye Mkurugenzi wa CMA Mhe. Usekelege Mpulla, ameipongeza kamati hiyo kwa kuendelea kutetea bajeti ya Tume hiyo bungeni na ameihakikishia kamati kuendelea kutekeleza maagizo