News
Kamati ya Bunge yaipongeza PSSSF uwekezaji wenye tija
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Fatma Toufiq ameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa uwekezaji wenye tija inaoufanya kupitia miradi ya maendeleo na utoaji huduma kwa wanachama.
Ametoa pongezi hizo leo Novemba 7, 2024 Bungeni Jijini Dodoma baada ya wataalam wa PSSSF kutoa wasilisho la hali ya uwekezaji wa mfuko huo na mwelekeo wa masuala ya uwekezaji.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri MKuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete ametoa wito kwa PSSSF kuendelea kutangaza miradi wanayoitekeleza ili wanachama na wananchi kwa ujumla watambue kazi zao.
Aidha, kikao cha Kamati hiyo kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mary Maganga, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Aneth Marthania, na Mkurugenzi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Festo Fute pamoja na watendaji wengine kutoka Ofisi hiyo.