Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ndejembi azindua mtandao wa Kitaifa wa Vijana "TK MOVEMENT"


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe Deogratius Ndejembi amezindua Mtandao wa Kitaifa wa Vijana wa Taifa Letu, Kesho Yetu (TK MOVEMENT) na kusema kuwa serikali imeendelea kushughulikia na kutafuta njia mbadala ya kutatua changamoto zinazowakumba vijana katika masuala ya ajira.

Mhe Ndejemvi amesema katika kushughulia changamoto hiyo wizara inaandaa ‘Innovation Hub’ ambapo kijana anaeamini kuanzisha biashara itakayosaidia wengine katika jamii atasaidiwa kuwezeshwa ili kumsaidia kutimiza azma ya biashara yake hiyo.

“ Tunaanza kuwa na innovation hub ambapo kijana anaeamini kuanzisha biashara itakayosaidia wengine katika jamii tutaanza kuwawezesha, tunafahamu kuwa ukiwa na wazo la biashara cha kwanza kinachokwamisha ni kodi ya pango, hivyo kupitia innovation hub hiyo kutawezesha kupunguza changamoto hiyo kwa vijana,” Amesema Mhe Ndejembi.

Aidha ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutoa hamasa na kipaumbele kwa vijana kuchangamkia fursa za ajira kwenye miradi ya maendeleo inayokua inatekelezwa kwenye halmashauri zao.

“ Niwapongeze sana TK Movement kwa kuja na wazo hili la kukutana na vijana wenzenu na kuwapa mafunzo ya namna ya kujikwamua kiuchumi kwa kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao. Ni wito wangu kwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuwapa ushirikiano pindi mtakapofika kwenye maeneo yao kutoa mafunzo kwa vijana.