Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Tanzania, China kuendelea kushirikiana kuwainua kiuchumi Vijana


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas katambi amesema Tanzania na China zitaendelea kushirikiana kuwainua kiuchumi vijana katika masuala ya Ajira na kazi ili kutoa fursa kushiriki katika ujenzi wa Taifa lao.

Mhe. Katambi amesema hayo Juni 5, 2024 wakati wa hafla ya miaka 60 ya mahusiano ya kirafiki baina ya nchi hizo mbili yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.

Aidha, amesema mahusiano mazuri yaliyopo yamesaidia kuongeza fursa za Ajira nchini, kutoa fursa ya kujifunza namna ya kutumia teknolojia na kuwasaidia vijana kujifunza namna ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.