Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Katambi Serikali inatambua mchango wa Wahandisi Vijana


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa Wahandisi Vijana katika kukuza maendeleo ya taifa, hivyo wataendelea kupatiwa ushirikiano ili kutimiza ndoto zao.

Amebainisha hayo Septemba 3, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua jukwaa la Wahandisi Vijana lililoandaliwa na ERB likiongozwa na Kauli mbiu isemayo "Kuwainua Vijana katika safari yao ya Taaluma na Biashara,"

Aidha, Mhe. Katambi amesema kuwa, wahandisi Vijana 25, 686 wamesajiliwa na Bodi ya Usajili Wahandisi katika kipindi cha Miaka Mitatu ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Miradi mingi ya maendeleo imeanzishwa ambapo serikali imetenga Shilingi Bil. 840 kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo na Wahandisi Vijana ni miongoni mwa watakao nufaika" amesema.

Sambamba na hayo, Mhe. Katambi amewasihi Wahandisi hao kutumia elimu na ujuzi walionao sio tu kutafuta Ajira bali kutengeneza Ajira kwa vijana wengine na kuendeleza ubunifu zao.

Katika Jukwaa hilo pia ameshiriki Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Zena Ahmed Said.