Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Vijana wahimizwa kuchangamkia fursa Miradi ya Kimkakati


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - kazi, Vijana, ,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi ametoa rai kwa Vijana nchini kutambua na kuchangamkia miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita ili waweze kunufaika kiuchumi na kuondokana na changamoto ya ajira.

Mhe. Katambi amebainisha hayo Mei 26. 2024 Jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa shindano la kutaja miradi iliyotekelezwa na serikali, maarufu “SAMA CHALLENGE U KNOW”.

Aidha, katika Shindano hilo imeshuhudiwa Mtoto mdogo mwenye umri wa miaka 7 aliyejitambulisha kama Profesa Baraka, akionesha uwezo wake wa kuitambua na kuielezea miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.