Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kamati ya Bunge yaridhishwa uendeshaji Rocy City Mall


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii leo tarehe 25 Mei, imeridhishwa na uendeshaji wenye tija wa Mradi wa PSSSF wa Jengo la Kitega Uchumi la Rock City Mall jijini Mwanza, ambapo jengo hilo limepangishwa kwa 88%.

Akiongea mara baada ya kukagua shughuli za Rocky City Mall, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Fatma Hassan Toufiq amebainisha kuwa kwa sasa jengo linao wapangaji wa kutosha na shughuli nyingine za kuongeza mapato ya mradi huo.

Akitoa ufafanuzi juu ya usimamizi wa serikali kwenye Mradi huo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Patrobas Katambi ameeleza kuwa maelekezo na ushauri wa kamati hiyo utaendelea kufanyiwa kazi ili mradi huo uendelee kuchochea uchumi wa jiji la Mwanza na Taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru amefafanua kuwa mfuko huo unaendelea na utekelezaji wa mipango ya kimkakati ya kuhakikisha mradi huo unaongeza mapato na kuvutia wafanyabiashara.