Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

IKUPA: VIJANA KUPATIWA UJUZI WA KITALU NYUMBA


Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na watu wenyeulemavu,Stella Ikupa, amezitaka halmashauri nchini kutoa elimu kwa vijana juu ya kilimo cha kitalu nyumba (Green House)

Naibu Ikupa aliyasema hayo Mkoani wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya kilimo cha kitalu nyumba (green house) huku akiipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Rombo kwa hatua waliyofikia katika utekelezaji wa mradi huo.

Alisema kuwa vijana wanatakiwa kutambua fursa zilizopo katika kilimo na watumie rasilima ardhi katika kujipatia ajira zitakazo wanufaisha wao pamoja na wenzao ambao wataweza kuwaajiri.

Mhe.Ikupa amesema kuwa vijana wanatakiwa kupatiwa elimu kuhusu umuhimu wa kilimo cha kitalu nyumba ili watambue kuwa kilimo kina faida na utajiri mkubwa sana.

“Vijana wanapenda kufanya kazi za ofisini pekee, kitu ambacho sio kweli, maisha hayapo kwenye kalamu pekee bali maisha yapo kwenye kilimo, ukimkuta mtu kafanikiwa kwenye kilimo ni zaidi ya yule aliyeko ofisini." alisema Ikupa.

Aidha, Waziri Ikupa alitaka halmashauri kuwa hamasisha na walemavu kushiriki katika vikundi hivyo vya vijana vitakavyonufaika na mradi huo, ili kuweza kupatiwa mikopo ambaye itawasaidi kuinua kipato chao.

Akiwa wilaya ya Rombo Naibu waziri Ikupa alitembelea eneo lililotengwa na Halmashauri ya Wilaya kwa ajili ya Ujenzi wa Kitalu Nyumba (Green House) ya mfano kwa ajili ya vijana kujifunzia zaidi mambo ya kilimo.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri Ikupa,alitembelea kituo cha Watoto wenye Ulemavu cha Mashima kilichopo Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro ambapo ameahidi kutatua changamoto zilizopo katika kituo hicho.