Announcement
Announcement for Apprenticeship Opportunity
- Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu inatekeleza Programu ya Kukuza Ujuzi Nchini inayowezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la ajira. Ofisi imeingia makubaliano vyuo mbalimbali kutoa mafunzo mafunzo ya ufundi stadi kukuza ujuzi na stadi za kazi kwa vijana. Miongoni mwa mafunzo yatakayotolewa ni Ubunifu wa Mitindo na Ushonaji Nguo, Ufundi Bomba, Uashi, Useremala, Uchomeleaji na Uungaji vyuma, Upakaji rangi na maandishi ya alama, Utengenezaji wa vipuri vya mitambo, Ufundi Magari na Mitambo, Umeme wa Majumbani na Viwandani, TEHAMA, Umeme wa Magari, Huduma za Hoteli na Utalii, Ukataji Madini ya Vito na Kilimo.
- Hivyo, tunapenda kuwatangazia vijana wa Kitanzania wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 wanaopenda kujiunga na mafunzo katika mojawapo ya fani zilizoorodheshwa hapo juu wafike katika vyuo vilivyoainishwa na Tangazo hili hapa chini ili kuchukua fomu ya kuomba kujiunga na mafunzo. Serikali itafadhili ada ya mafunzo kwa asilimia 100. Mwanafunzi / mzazi / mlezi atagharamia gharama nyingine zikijumuisha nauli ya kwenda chuoni na kurudi nyumbani. Mafunzo yatakayotolewa ni ya kutwa hivyo mwombaji anashauriwa kuomba mafunzo haya katika chuo kilicho katika Mkoa anaoishi.
- Maombi yawasilishwe kuanzia tarehe 01/11/2023 hadi tarehe 14/11/2023 yakiambatana na nyaraka zifuatazo:
i. Barua ya maombi ya mafunzo;
ii. Nakala ya Cheti cha kuzaliwa;
iii. Nakala ya Cheti cha elimu uliyohitimu ;
iv. Kitambulisho cha uraia / kadi ya mpiga kura (Kwa wenye miaka 18 na kuendelea);
v. Barua ya utambulisho kutoka Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Kijiji anakoishi mwombaji; na
vi. Picha nne za paspoti (ziandikwe majina matatu ya mwombaji kwa nyuma).
4. Sifa za kujiunga na mafunzo haya ni:
i.Elimu ya msingi au zaidi kwa fani za ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo, ufundi bomba, ujenzi, useremala, uchomeleaji na uungaji vyuma, upakaji rangi na maandishi ya alama;
ii.Elimu ya kidato cha nne na kuendelea kwa fani nyingine zilizobaki zikijumuisha fani ya utengenezaji wa vipuri vya mitambo, ufundi magari, umeme wa majumbani na viwandani, TEHAMA, umeme wa magari na umeme wa jua (solar);
iii.Awe Mtanzania;
iv.Awe na umri kati ya miaka 15 – 35;
v.Awe mwenye afya njema;
5. Vijana wa Kike na Vijana Wenye Ulemavu wanasisitizwa kuomba fursa hizi na watapewa kipaumbele katika nafasi za mafunzo haya;
6. Maombi yachukuliwe na kuwasilishwa kwenye vyuo vilivyo katika Mkoa wako ambavyo vimekubaliwa na Serikali kutoa mafunzo haya; na
7. Watakaokidhi vigezo na sifa tu ndio watakaochanguliwa
Tangazo hili linapatikana katika Tovuti ya Ofisi (www.kazi.go.tz)
IMETOLEWA NA:
KATIBU MKUU
01/11/2023
NB: Fomu za maombi zinapatikana katika vyuo vyote vilivyopitishwa na Serikali kutoa mafunzo haya.
VYUO VILIVYOKUBALIWA KUTOA MAFUNZO YA UANAGENZI
NA | MKOA | WILAYA | JINA LA CHUO | FANI |
1 | Arusha | Arusha Jiji | Don bosco KII - TECH | Umeme jua |
ufundi umeme | ||||
Karatu | Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mto wa Mbu | Uongozaji Watalii | ||
Ufundi Bomba | ||||
Umeme wa Majumbani | ||||
2 | Dar es salaam | Temeke | Dsm RVTSC | Ufundi Magari |
Ufundi wa kutengeneza vifaa kutumia Aluminium | ||||
Ufundi Bomba | ||||
Umeme wa Majumbani | ||||
Uchomeleaji na Uungaji vyuma | ||||
Ukarabati wa bodi za magari | ||||
Ufundi Umeme wa Magari | ||||
Ushonaji | ||||
Kinondoni | Don bosco Oysterbay VTC | Ufundi magari | ||
Useremala | ||||
Uchomeleaji na uungaji vyuma | ||||
Uchorongaji vipuri | ||||
Ushonaji | ||||
3 | Dodoma | Dodoma | Instistute of Heavy Equipment and Technology (IHET) | Ufundi wa mitambo |
Uchomeleaji na uungaji vyuma | ||||
Umeme wa magari | ||||
Don Bosco Dodoma Technical Institute | Useremala | |||
Ufundi bomba | ||||
Uashi | ||||
Uchomeleaji na uungaji vyuma | ||||
Ufundi magari | ||||
Uchorongaji vipuri | ||||
Ufundi umeme | ||||
Ushonaji | ||||
Umeme jua | ||||
4 | Geita | Geita | Geita VTC | Umeme Majumbani |
Ufundi Magari | ||||
Ufundi Bomba | ||||
Uashi | ||||
5 | Iringa | Iringa | Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Ilula | Umeme wa majumbani |
Useremala | ||||
Ushonaji | ||||
Uchomeleaji na uungaji vyuma | ||||
Mufindi | Mafinga Lutheran Vocational Training Centre | Ufundi magari na Mitambo | ||
Uchomeleaji na Uungaji wa Vyuma | ||||
Useremala | ||||
Ushonaji | ||||
Kilolo | RDO Kilolo VTC | Umeme wa Majumbani | ||
Upishi | ||||
Ushonaji | ||||
Useremala | ||||
Uashi | ||||
6 | Kagera | Biharamulo | Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Rubondo | Umeme wa majumbani |
Ufundi magari | ||||
Ushonaji | ||||
Uashi | ||||
Misenyi | Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Gera | Ufundi umeme | ||
Uashi | ||||
Kilimo | ||||
7 | Katavi | Mpanda | Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Msaginya | Umeme wa Majumbani |
Useremala | ||||
Ushonaji | ||||
Kilimo | ||||
8 | Kigoma | Kasulu | Kasulu DVTC | Ufundi umeme wa majumbani |
Uashi | ||||
Ufundi Magari | ||||
Ushonaji | ||||
Kasulu | Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kasulu | Ufundi umeme wa majumbani | ||
Uchomeleaji na uungaji vyuma | ||||
Umeme wa magari | ||||
Ufundi bomba | ||||
Ushonaji | ||||
Ufundi magari | ||||
Kakonko | Chuo cha Ufundi Stadi JKT Kasanda | Ufundi bomba | ||
Ufundi umeme | ||||
Upishi | ||||
Ushonaji | ||||
Ufundi magari | ||||
Kigoma Vijijini | Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kihinga | Umeme wa majumbani na viwandani | ||
Uashi | ||||
Ushonaji | ||||
9 | Kilimanjaro | Moshi Vijijini | Marangu School of Tourism and Vocational Training | Kuongoza watalii |
Upishi | ||||
Huduma za kupokea wageni | ||||
Huduma za vyakula na vinywaji | ||||
Rombo | Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mamtukuna | Uashi | ||
Useremala | ||||
Ufundi Magari | ||||
Umeme wa Majumbani | ||||
10 | Lindi | Kilwa | Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko | Umeme wa majumbani |
Ushonaji | ||||
Ufundi Magari | ||||
Kuongoza Watalii | ||||
Ruangwa | Ruangwa DVTC | Ufundi umeme wa majumbani | ||
Uashi | ||||
Ushonaji | ||||
Ufundi magari | ||||
11 | Manyara | Mbulu | Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Tango | Umeme wa majumbani |
Useremala | ||||
Ufundi magari | ||||
Ushonaji | ||||
Uashi | ||||
12 | Mara | Musoma | St. Anthony Vocational Training Centre | Ushonaji |
Ufundi magari | ||||
Uchomeleaji na uungaji vyuma | ||||
Umeme wa magari | ||||
13 | Mbeya | Mbeya Mjini | Chuo cha Ufundi Magereza Ruanda | Useremala |
Uashi | ||||
Umeme wa majumbani | ||||
Ushonaji | ||||
Uchomeleaji na uungaji vyuma | ||||
14 | Morogoro | Morogoro | Lakewood Training Institute | Umeme wa majumbani |
Kuongoza watalii | ||||
15 | Mtwara | Masasi | Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Masasi | Umeme wa majumbani |
Ushonaji | ||||
Ufundi bomba | ||||
Uashi | ||||
Uchomeleaji na uungaji vyuma | ||||
16 | Mwanza | Ilemela | Mwanza RVTSC | Uchomeleaji na Uungaji vyuma |
Ufundi Umeme wa Majumbani | ||||
Useremala | ||||
Ufundi wa uchanganyaji na upakaji rangi | ||||
Ginnery Fitting | ||||
Ufundi magari | ||||
Ufundi Bomba | ||||
Sengerema | Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Sengerema | Ufundi Umeme | ||
Uchomeleaji na Uungaji vyuma | ||||
Ufundi magari | ||||
Ushonaji | ||||
Uashi | ||||
17 | Njombe | Njombe | Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Njombe | Umeme wa majumbani na viwandani |
Ushonaji | ||||
Ufundi magari na mitambo | ||||
Uchomeleaji na uungaji vyuma | ||||
Uashi | ||||
18 | Pwani | Kibaha | Pwani RVTSC | Ufundi umeme wa majumbani |
Useremala | ||||
Ufundi umeme wa magari | ||||
Utengenezaji wa friji na Viyoyozi | ||||
Ushonaji | ||||
Ufundi magari | ||||
19 | Rukwa | Sumbawanga | LAELA AGRICULTURE VTC | Kilimo cha mbogamboga (Horticulture) |
Ufugaji (Animal Husbandry) | ||||
Sumbawanga | Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST - Rukwa) | Uchomeleaji na Uungaji vyuma | ||
Uashi | ||||
Ufundi bomba | ||||
Ufundi Umeme wa Majumbani na Umeme Jua | ||||
20 | Ruvuma | Mbinga | Chuo cha Ufundi Stadi Mpapa | Useremala |
Ushonaji | ||||
Umeme | ||||
Uchomeleaji | ||||
Songea vijijini | Peramiho Vocational Training Center | Ushonaji | ||
Ufundi Bomba | ||||
Useremala | ||||
Ufundi Magari | ||||
Umeme wa Majumbani | ||||
21 | Shinyanga | Kahama | Hill Forest College - Kahama | Front Office Operations |
22 | Simiyu | Bariadi | Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bariadi | Umeme wa majumbani |
Ufundi magari | ||||
Uchomeleaji na uungaji vyuma | ||||
Ushonaji | ||||
Uashi | ||||
Useremala | ||||
23 | Singida | Singida Mjini | Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu Sabasaba | Umeme wa Majumbani |
Ushonaji Nguo | ||||
Ususi na Urembo | ||||
Uchomeleaji | ||||
Uokaji keki na mikate | ||||
Singida mjini | Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Singida | Ufundi umeme | ||
Ufugaji | ||||
Useremala | ||||
Ushonaji | ||||
Ufundi magari | ||||
24 | Tabora | Urambo | Urambo DVTC | Ushonaji |
Uashi | ||||
Ufundi umeme wa majumbani | ||||
Nzega | Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mwanhala | Umeme wa majumbani | ||
Ufundi magari | ||||
Ushonaji | ||||
Uashi | ||||
25 | Tanga | Lushoto | St. Patrick's Vocational Training Centre | Ufundi Magari |
Useremala | ||||
Ushonaji | ||||
Umeme wa magari | ||||
Umeme wa majumbani | ||||
Handeni | Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Handeni | Ufundi umeme wa majumbani | ||
Ufundi magari | ||||
Upishi | ||||
Ushonaji | ||||
Uchomeleaji na uungaji vyuma |