Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

Biography

Ms. Mary Ngelela Maganga
Ms. Mary Ngelela Maganga
Permanent Secretary, Prime Minister's Office (Labour, Youth, Employment & Persons With Disability)

Bi. Mary Ngelela Maganga ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu. Aidha, ameshika nyadhifa mbalimbali katika utumishi wa Umma zikiwemo Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira); Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Huduma za Hazina na Kamishna wa Bajeti katika Wizara ya Fedha na Mipango; Mkurugenzi wa Utafiti, Sera na Mipango; Meneja wa Programu ya Kuboresha Usimamizi wa Kodi na Mkuu wa Kitengo cha Mipango katika Mamlaka ya Mapato Tanzania; na Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Posta Tanzania.

Aliwahi kuwa Mjumbe wa Bodi katika Benki Kuu ya Tanzania; Msimamizi wa Tathmini ya Uchunguzi wa Utawala na Usimamizi Kodi katika Mamlaka ya Mapato Tanzania; Mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya Jukwaa la Usimamizi wa Kodi la Afrika na Mtaalam Mshauri wa Shirika la Fedha la Umoja wa Mataifa (IMF) katika kuandaa na kutekeleza Mipango Mikakati ya Kuboresha Usimamizi wa Kodi katika nchi za Ethiopia, Ghana, Malawi, Nigeria, Rwanda, Zambia na katika Bodi ya Mapato Zanzibar.

Bi Mary Ngelela Maganga, ana Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Southern Illinois (Marekani) na Shahada ya Kwanza ya Sanaa katika Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.