Msajili wa Vyama Vya Wafanyakazi

MSAJILI WA VYAMA HURU VYA WAFANYAKAZI NA WAAJIRI

Ofisi ya Msajili ilianzishwa kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa haki ya msingi inayohusu haki na uhuru wa kujumuika na kuanzisha Vyama vya wafanyakazi na Waajiri; wavipendavyo na kwa hiari yao wenyewe kama ilivyoelekezwa katika Mikataba Na. 87 na 98 ya Shirika la Kazi Duniani (ILO).

Majukumu ya Ofisi ya Msajili ni:-

  • Kushughulikia masuala yote yanayohusu usajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri pamoja na Mashirikisho yao kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Na. 6 ya 2004
  • Kutoa ushauri kwa wadau juu ya taratibu na masuala ya kuzingatiwa wakati wa kuanzishwa kwa Vyama hivyo.
  • Kusimamia na kuratibu shughuli za Vyama kama vile kufanya kaguzi za kisheria zinazohusu rejista za Wanachama na kuona kuwa michango ya Wanachama inatumika vizuri kwa malengo ya kivyama
  • Kusimamia matumizi ya Katiba na Kanuni, hususan malalamiko yanayotokana na ukiukwaji wake na kutoa maelekezo kwa wadau
  • Kuelimisha Wadau juu ya haki ya msingi ya kujumuika/kuanzisha chama na majukumu na wajibu wa vyama vinavyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Na. 6 ya 2004