Idara ya Sera na Mipango

Idara hii ina jukumu la kuratibu utayarishaji wa sera, sheria na mipango mbalimbali ya Wizara, pamoja na kusimamia na kutathmini utekelezaji wake.

Idara hii inahusika na kuratibu ubunifu, uandaaji, ukamilishaji na utekelezaji wa sera, mikakati, programu na miradi ya Wizara na kuratibu uandaaji wa makisio ya mapato na matumizi (Bajeti) ya Wizara na hotuba ya bajeti na kuziwasilisha katika mamlaka zinazohusika.

Aidha, inawajibika kutoa ushauri na miongozo ya kitaalam kwa idara mbalimbali zilizo chini ya Wizara kuhusu masuala ya sera na mipango.