Idara ya Ajira

Idara ya Ajira ni miongoni mwa Idara Kuu tatu za Wizara ya Kazi na Ajira.

Idara hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu:

1.Sehemu ya Huduma za Ajira (Employment Services Section)

Sehemu ya Huduma za Ajira hutoa huduma mbalimbali za ajira kwa wananchi ili kusaidia kukua kwa uchumi na kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa Watanzania. Sehemu hii ina majukumu yafuatayo:-

· Kukusanya, kuandaa na kutoa taarifa kwa Umma juu ya hali ya soko la ajira

· Kufuatilia hali ya soko la ajira na kushauri taasisi za elimu za Umma na binafsi juu ya mapengo ya ujuzi wa wahitimu wao

· Kusajili, kufuatilia na kusimamia shughuli za wakala binafsi za huduma za ajira

· Kuratibu utoaji wa vibali vya ajira za wageni na kufuatilia mienendo yao katika ajira zao. Waajiri ndio wanaowajibika kuwaombea wageni vibali vya ajira za wageni na katika kufanya hivyo maombi yao yanazingatia kujaza fomu maalumu (TIF 1)

· Kusimamia na kuratibu urithishaji ujuzi/utaalamu wa wageni kwa wazalendo(Tranzfer skills)


2.Sehemu ya Taarifa za Soko la Ajira (Labour Market Information Section)

Jukumu kuu la sehemu hii ni kuratibu tarifa za soko la ajira hapa nchini.

 Kazi za Sehemu ya taarifa za soko la Ajira ni:-

 • Kushirikiana na wadau katika kufanya tafiti na mafunzo juu ya soko la ajira, kuchambua na kutoa taarifa kwa wahusika
 • Kuratibu ukusanyaji takwimu na taarifa za soko la ajira kwa ajili ya utekelezaji  wa masuala ya kisera na uandaaji wa mipango
 • Kushirikiana na shirika la takwimu la Taifa na wadau wengine katika kukusanya takwimu mbali mbali zinazohusu ajira na kazi
 • Kufanya marekebisho ya kamusi ya kazi na kuratibu matumizi yake
 • Kufuatilia mwenendo wa ajira na kupata  taarifa za soko la ajira ili kubainisha maeneo ambayo yatahitaji mafunzo maalum au tafiti.
 • Kuratibu miongozo, viwango na mifumo ya kukusanya, kuchambua na kutangaza takwimu na tarifa za soko la ajira kwa kushirikiano na Ofisi ya Taifa ya Takwimu
 • Kupanga na kuandaa ufuatiliaji au utafiti kwa kushirikiana na kitengo cha  Ukuzaji wa ajira na taasisi za utafiti
 • Kukusanya na kuchambua na kuwasilisha tafiti na usimamizi wa soko la ajira  kutoka idara, na taasisi binafsi
 • Kupanga, kundaa, na kuunganisha tafiti za soko la ajira kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
 • Kuratibu mafunzo ya taarifa za soko la ajira.
 • Kuandaa programu kwa ajili ya uingizaji wa taarifa, utayarishaji na uchambuzi wa takwimu za kazi na ajira.
 • Kuandaa na kutengeneza huduma za tovuti kwa ajili ya idara ya ajira.

3.Sehemu ya Ukuzaji Ajira (Employment Promotion Section)

Jukumu kubwa la Sehemu ya Ukuzaji Ajira ni kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa Watanzania.

Katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa wananchi sehemu hii ina majukumu yafuatayo:-

 • Kuendeleza sekta isiyo rasmi, ili kuwawezesha kukua na kuingia katika sekta kubwa inayo toa mchango katika pato la Taifa.
 • Kuratibu utoaji wa ujuzi wa kuwaongezea wananchi uwezo wa kujiajiri.
 • Kushauri wadau kutoa vipaumbele vya ajira kwa makundi maalum, yaani kwa kuangalia wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kujiajiri.
 • Kushauri wadau kuweka mazingira yanayokuza ajira rasmi na ile isiyo rasmi.
 • Kushauri halmashauri husika kutenga maeneo ya kufanyia biashara.
 • Kufuatilia na kutoa tathimini ya mwenendo wa ajira katika sekta rasmi na ile isiyo rasmi.Taarifa hizi husaidia kupata mwelekeo wa jinsi ajira inavyo kua kwa kulianganisha na ongezeko la watu wanaoingia katika soko la ajira.
 • Kushauri juu ya sera za uchumi jumla kuhusu ukuzaji wa ajira, ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa kupata mikopo.
 • Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa sera ya Taifa ya ajira.
 • Kuandaa, kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa sera, sheria na kanuni zenye lengo la kukuza ajira.
 • Kukuza na kuratibu shughuri za sekta isiyo rasmi ili kuongeza ajira. Katika hili wizara imekuwa ikiratibu maonesho ya Nguvukazi/Juakali yanayo washirikisha wajasiriamali wote wanchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 • Kuratibu utekelezaji wa mafunzo ya kujiajiri na kuondoa umaskini (Demand Driven Skills Training Programme).