Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

WATAALAMU WA NCHI WANACHAMA SADC KUJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA SEKTA YA KAZI NA AJIRA


Wataalamu wa Sekta ya Kazi na Ajira kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika wamedhamiria kuboresha na kuendeleza sekta ya kazi na ajira kwa kutatua changamoto zilizopo katika sekta hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ufunguzi wa mkutano SADC wa wataalamu wa utatu sekta ya kazi na ajira Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe alieleza kuwa mkutano huo umewakutanisha kwa ajili ya kuangalia namna ya kuboresha sera za sekta ya kazi na ajira ambazo zitachangia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira.

“Mustakabali wa sekta ya kazi na ajira unategemea jinsi ambavyo tunashughulikia fursa na changamoto zitokanazo katika mazingira ya sekta hiyo, hivyo mada zitakazo jadiwa katika mkutano huu zitatoa mwelekeo kwa wajumbe kuona namna ya kuwa na sera rafiki za kazi na ajira,” alieleza Massawe

Alifafanua kuwa kulingana na taarifa ya mwenendo wa ajira ulimwenguni ya mwaka 2019 iliyotolewa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) imeelezea hali ya ajira inayoonesha zaidi ya watu milioni 170 hawana kazi ikiwa ni sawa na asailimia 5.1, na wafanyakazi bilioni 2 wapo katika ajira isiyo rasmi ikiwa ni sawa na asilimia 61.2.

“Ni matumaini yangu ajenda zitakazo jadiliwa zitatoa mwelekeo wa namna bora ya kutatua changamoto zilizopo sasa na mapendekezo yatakayotolewa na wataalamu kutoka nchi wanachana yatakuwa yanazingatia vipaumbele na malengo endelevu katika sekta ya kazi na ajira,” alisema Massawe

Sambamba na hayo alieleza kuwa Serikali imeendelea kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa kutoa elimu ya sheria za kazi ili kuongeza uelewa kwa wananchi kufanya kazi zenye staha na kuboresha mazingira ya kazi.

Akitolea mfano Ofisi ya Waziri Mkuu inavyotekeleza Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika kuwezesha vijana ambao ndio nguvukazi ya taifa wanavyoshiriki katika kufanya kazi za staha kupitia mafunzo wanayopatiwa chini ya programu hiyo.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Kijamii na Rasilimali Watu Bi. Duduzile Simelane alieleza kuwa ukuaji wa sayansi na teknolojia umechangia kwa kiasi kikubwa nchi wanachama za SADC kukuwa kiuchumi hivyo kumekuwa na hitaji la kuwa na miongozo sahihi, sera na sheria zitakazo wawezesha kushirikiana kwa pamoja katika kukuza sekta ya kazi na ajira.

Naye, Mwenyekiti wa Shirikisho la Waajiri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Dkt, Aggrey Mlimuka alisema kuwa ajenda zitakazojadiliwa zitatoa fursa kwa nchi wanachama kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo kwa wafanyakazi ambao ni chachu ya ukuaji uchumi.

Mkutano huo unafanyika kwa siku tano kuanzia tarehe 18 hadi 22 Novemba, 2019 na umeshirikisha wajumbe kutoka nchi ya Angola, Botswana, Eswatini, Malawi, Msumbiji, Lesotho, Afrika Kusini, Namibia na Zimbabwe. Wajumbe wengine kutoka Shirika la Kazi Dunianai (ILO), SATUCC, SPSF, Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), ZANEMA na ZATUC.