Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Naibu Katibu Mkuu Zuhura Afungua Mafunzo ya PD-MIS


✅ Awataka Wakurugenzi wa Halmashauri kutenga Bajeti kuwezesha Mfumo wa PD-MIS

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Zuhura Yunus ametoa wito kwa Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhakikisha inasimamia Maafisa Ustawi wa Jamii waliopata mafunzo ya Mfumo wa Kielektroniki wa taarifa na kanzidata kwa Watu wenye Ulemavu (PD-MIS).

Aidha, amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri wazingatie kutenga bajeti mahususi kwa ajili ya kuwezesha matumizi endelevu ya Mfumo wa PD-MIS.

Bi. Zuhura amebainisha hayo Julai 16, 2025 Mkoani Tabora wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Mfumo wa PD-MIS kwa washiriki kutoka Miko na Halmashauri za Kanda ya Magharibi.

Katika hatua nyingine, amewahimiza Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia kikamilifu matumizi ya Mfumo huo ndani ya maeneo yao ili kuhakikisha Watu Wenye Ulemavu wananufaika na huduma zinazotolewa na serikali pamoja na wadau.

Awali akizungumza Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu, Ofisi hiyo Bw. Rasheed Maftah, amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wa kutumia PD-MIS, ili watakaporudi ofisi waanza kutumia mfumo huo kuwasajili wenye ulemavu na kuwaunganisha na huduma stahiki.

Kwa upande wake Mwakilishi Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi. Amina Faki ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yataongeza tija na ufanisi katika kutoa huduma kwa Watu wenye Ulemavu kwa kutambua wako wapi, wanahitaji huduma ipi na wanasaidiwaje.