Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

MENEJIMENTI YA OFISI YA WAZIRI MKUU YAPATIWA MAFUNZO YA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA


Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imepatiwa mafunzo na Wataalamu kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya mwaka 2011 na mabadiliko yake ya mwaka 2016 ili kuwajengea uwezo zaidi katika suala la ununuzi na kusimamia mikataba ya ununuzi wa umma pamoja na kuhakikisha mikataba inayoingia baina ya Ofisi na Wazabuni haileti kasoro yoyote.

Mafunzo hayo yamefanyika hii leo Oktoba 20, 2020 katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la PSSSF, Jijini Dodoma.