News
Maafisa Kazi watakiwa kuwa wabunifu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amewaagiza Maafisa Kazi Wafawidhi nchini kuendeleza ubunifu katika utendaji wao wa kazi huku wakizingatia maadili ya utumishi wa umma.
Amewasisitiza kutoa huduma bora na kwa wakati hususani katika maeneo nyeti yanayohusisha usuluhishi wa migogoro ya kikazi na malalamiko ya wananchi mara yanapofikishwa kwenye ofisi zao.
Waziri Ridhiwani alieleza hayo Septemba 12, 2025 mkoani Morogoro wakati wa Kikao kazi cha kuandaa mwongozo wa ukaguzi mahali pa kazi ili kujumuisha masuala ya wafanyakazi wa Nyumbani, Watu wenye Ulemavu na Utumikishwaji wa Mtoto.
Katika hatua nyingine, amewataka Maafisa hao kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa jamii kwa kushirikiana na wadau wa Utatu amba oni Serikali, vyama vya waajili ana vyama vya wafanyakazi katika kushughulikia changamoto za kikazi.
Kikao hicho kiliwahusisha viongozi wa Idara ya Kazi, Msajili wa Vyama Vyama vya Wafanyakazi, pamoja na Maafisa Kazi Wafawidhi wa Mikoa yote Tanzania.