Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

BARAZA LA TAIFA LA USHAURI KWA WATU WENYE ULEMAVU WAKUTANA NA KUJADILI MASUALA MBALIMBALI KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU


Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Ushauri kwa Watu wenye Ulemavu Dkt. Lukas Kija (kushoto) akizungumza na wajumbe wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha kwa ajili ya kujadili masula mbalimbali ya Watu wenye Ulemavu. Kulia ni Bi. Christina Mero mjumbe wa Baraza hilo.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Ushauri kwa Watu wenye Ulemavu Dkt. Lukas Kija akiongoza kikao hicho kilichofanyika Februari 24, 2020, Jijini Dodoma.

Sehemu ya Wajumbe wa baraza hilo wakifuatilia kwa makini hoja mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la PSSSF, Jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Taifa la Ushauri kwa Watu wenye Ulemavu Bw. Jacob Mwinula akieleza jambo wakati wa kikao kazi hicho kazi kilichowakutanisha kwa ajili ya kujadili masula mbalimbali ya Watu wenye Ulemavu.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Taifa la Ushauri kwa Watu wenye Ulemavu wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakiwasilishwa na Katibu wa Baraza hilo (hayupo pichani). Wa pili kutoka kushoto ni Mkalimani wa Lugha ya alama Bw. Adrian Chiyenje.

Mjumbe wa Baraza la Taifa la Ushauri kwa Watu wenye Ulemavu Bw. Peter Charles akichangia mada wakati wa kikao kazi hicho.

Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Taifa la Ushauri kwa Watu wenye Ulemavu wakipitia taarifa wakati wa kikao kazi hicho kilichowakutanisha kwa ajili ya kujadili masula mbalimbali ya Watu wenye Ulemavu.